Makala
SIKU 7 ZA KUANGUSHA ROHO YA UZINZI MAISHANI
| Makala
SIKU 7 ZA KUANGAMIZA ROHO ZA UZINZI MAISHANI MWAKO:
Shalom mtu wa Mungu na jina la Bwana Yesu lihimidiwe sana;
Tunamshukuru sana Mungu ametupa kibali tena cha kuingia katika ratiba nzuri ya kutengeneza mambo yetu kiroho zaidi kwa njia ya Mfungo wa madhabahuni,
Tunaanza Mfungo wetu ambao utadumu kwa siku saba {7} pekee,kuanzia jumatatu ya tarehe 19 Febr mpaka jumapili ya tarehe 25 jumapili.
Ratiba hii inatokana na muendelezo wa mafundisho na maombi kwa habari ya roho ya uzinzi kwenye maisha ya muamini.
Kwa sababu Roho Mtakatifu ameliruhusu jambo hili kufanyika hapa madhabahuni, hakikisha kabisa haupitwi na jambo hili lenye kubadilisha historia ya maisha yako,
Roho ya uzinzi ina athari mbaya nyingi sana kuanzia kiroho mpaka kimwili na lengo kuu la shetani ibilisi kila mara anapoachilia hii roho kwa watu mbalimbali, analenga kuangamiza kesho za watu, maana yake ni kwamba leo hii unaweza kujisifia wewe ni kijana bora ama binti bora na huenda hakuna kama wewe, lakini ni mpango wa shetani usiwaze kesho yako ili aiangamize kabisa na wewe usifikie hatma nzuri ya maisha yako,
Kitaalam hii tunaiita ni CODE au PASSWORD muhimu ya kubadili majira katika maisha yako, maana kwa siku hizi 7{saba} tutahakikisha kila siku tunaingia katika maombi ya kuangusha na kuharibu kila:
1} Ngome ya adui kwenye maisha yako
2} Pando la adui lisilofaa maishani mwako
3} Agents wa adui maishani mwako {wanaotumwa na shetani kukuharibia mambo yako}
4} Mazingira hatarishi yanayonyonya nguvu za kiroho maishani mwako
5} Laana za kurithi au kutamkiwa kwa midomo ya wengine
6} Migogoro isiyoisha wala kusuluhishwa ndani ya mahusiano yenu
7} Kufuta hati zote za mashitaka juu yetu kwa damu ya Yesu Kristo
Kila siku tutakuwa tunakutana Madhabahuni kwa njia ya mtandao na tutahakikisha tunafundishwa vyema na Roho Mtakatifu na baada ya maarifa hayo tunaingia kwenye maombi maalum ya kujinasua katika roho hii chafu ambayo imemwagwa duniani kuharibu mahusiano mbalimbali.
Youtube Channel yetu ni SIRI ZA BIBLIA
Mawasiliano ya kujiunga kwenye group la Whatsapp la maombi zaidi na ushauri +255 758 708804 popote duniani tunakuhudumia.
Kila siku ya Mfungo nitakupatia maelekezo maalum hapa hapa ya kuikabili siku kwa njia kuu zifuatazo:
A} Mistari maalum ya kusoma katika mfungo huu
B} Namna ya kulitafakari neno unalolisoma kwenye biblia
C} Maombi ya ukiri na kutamka kwa kinywa chako ushinde
Pastor Innocent Mashauri
Madhabahu ya siri za biblia
Maarifa ya ki-Mungu
+255 758 708 804
SADAKA